HomeBiashara

Vodacom yaongeza muda wa kuuza hisa

Vodacom yaongeza muda wa kuuza hisa
Like Tweet Pin it Share Share Email
Vodacom yaongeza muda wa kuuza hisa
 
Dar es Salaam April 19, 2017: Akiongea jijini Dar es Salaam mapema leo,Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia alisema “Vodacom Tanzania PLC inatarajia kupokea maombi mengi ya kununua hisa katika kipindi cha wiki hii.Pia kutokana na ushauri kutoka Serikali ya Tanzania na  makundi mbalimbali muhimu ya kijamii yanayohitaji kuwekeza wakiwemo Wabunge,makundi ya watumishi wa kada mbalimbali wa serikali na maofisa wa vyama  vya Ushirika kutoka  sehemu mbalimbali za nchi,tumewasilisha maombi na kupata idhini kutoka Mamlaka ya Soko la mitaji na dhamana(CMSA) kuongeza muda wa zoezi la kuuza hisa kwa kipindi cha wiki tatu hadi kufikia Alhamisi ya tarehe 11,Mwezi Mei,2017.Mkurugenzi huyo alisema kuongezeka kwa muda wa mwisho wa kununua hisa utawezesha wanaohitaji kununua hisa  kwa makundi binafsi na taasisi zilizoomba muda uongezwe kushiriki kikamilifu katika mchakato huu.Tunatoa shukrani za dhati kwa watanzania ambao wamejitokeza kuwekeza kupitia kununua hisa na tunawakaribisha ambao bado hawajanunua hisa kuchangamkia fursa hii katika kipindi cha muda mfupi wa nyongeza.Mgawanyo na mchanganuo wa umiliki wa hisa inapendekezwa utafanyika kuanzia Mei 19,2017 na kuendelea kabla ya kumaliza mchakato wa mwisho wa kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam katika tarehe iliyopangwa ya Juni 6,2017.”
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati alipokuwa akitangaza kwa kampuni yao kuongeza muda wa zoezi la kuuza hisa kwa kipindi cha wiki tatu hadi kufikia Alhamisi ya tarehe 11,Mwezi Mei,2017.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano huo.

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.