HomeShosti talk

Utajuaje Kama Mahusiano Uliyonayo Yatadumu.

Utajuaje Kama Mahusiano Uliyonayo Yatadumu.
Like Tweet Pin it Share Share Email

Dalili 8 zitakuonyesha kama upo kwenye mahusiano ya kudumu au hapana.

Afya. Wote tunafikiria kuhusu hili. hasa kwa kadri tunavyoendelea kukua , tunatembelea madaktari, tunakula vizuri wakati mwingine. Tunatafuta dalili  na wakati mwingine matokeo yake  yanatuambia kuwa hali zetu sio nzuri.

Lakini tunapofikiria afya,  tunafanya hivyo katika miili yetu tu. mara nyingi tunasahau kufikiria kuhusu afya ya mahusiano na mapenzi.

Tunaangalia zaidi afya ya mwili katika maisha ,lakini kuwa na afya nzuri katika mahusiano ni  vitu vinavyoungana.

Kwa kurahisisha , mahusiano mabaya hayadumu. au  ingawa  yanaweza kukaa kwa muda fulani.Na kama yakidumu , atakuwepo mtu wa kuumia.

Lakini ni nini hasa afya ya mahusiano? Tutajuaje kama mahusiano yetu yatadumu?  Utajuaje kama uko na mtu sio sahihi, mtu ambaye mtaishia kwenye kona fulani tu?

Hakuna kipimo halisi cha kujua. Hakuna kipima joto  kinaweza kupima kiasi cha muda wa mahusiano  kuwa ni ya moto au baridi.

Kwa bahati kuna  hizi dalili 8 ambazo zinaweza kukusaidia kujua  afya iliopo kwenye mahusiano yako.

1.Mchumba wako atakuwa na imani na wewe , na wewe utakuwa na imani naye.

360nobscouples-740x431 Utajuaje Kama Mahusiano Uliyonayo Yatadumu

Hataongea kwa ajili yake bali ataongea kwa ajili yenu wote. atakukumbusha pale unapokuwa umesahau au unapokuwa na mashaka kwa jinsi ulivyo.  Ana  maono ya wazi ya muhimu kwako. atalea hali hio na utaiona. Vilevile na upande wako utakuwa kama yeye. hutamsema vibaya kwa marafiki, hutalalamika   kitu bali utaongea mbele yake. Utamwamini kuwa yuko kamili , mtu anayeweza kutatua matatizo na kusimama kwa miguu yake. Hata kama haujamsaidia kitu.

2.Unamwamini.

Unamwamini katika ukweli wake wote. ahadi zake ni za kweli.  utamkubali alivyo. Anahusika katika majukumu yake.

3.Unakubali mambo yake yaliopita na yeye anakubali ya kwako.

Jinsi alivyokuwa, alikuwa na wanawake wangapi,  wanaume wangapi. hutajali. utamkubali alivyo ili mkue pamoja.  hutafikiria kitu chochote kilichopita, bali utakuwa na hamu ya kutaka kujua  jinsi gani huyo mtu alivyo. Mahusiano yako yatakuwa yamekusanya, Msamaha  na kuachilia yaliopita.

4.Unashukuru kwa vitu vizuri mlivyonavyo

Unakubaliana na vitu vidogo vidogo anavyovifanya kwako.   unakuwa na matumaini,  husubiri kupata kazi, kwa ajili ya mshahara, kwa ajili ya mambo mengine. unashukuru kwa kile mlichonacho sasa na mwenza wako.

Mnafuraha wakati huu.  hana mchezo wa kijinga. anatengeneza pesa ya kutosha. anafanya kitu akipendacho. Utakuwa unalenga safari sio mwisho wa ndoa, mtoto,  sherehe,  vitu vinatokea kwa kawaida.

5.Mawasiliano ni ya wazi na ya kueleweka kwa kila mmoja.

Hakuna wa kusubiri ni nani atamtafuta mwenzake. kila mtu anakuwa na jukumu la kufanya hivyo. Na kama itatokea mmoja hakuhusika , hakuna lawama, kwa kuwa mnaelewa . utavaa moyo wake. hutahangaika kuyatawala mahusiano kwa sababu hamfanyi mchezo wa kuigiza.

6.Maisha yenu ya sex yataendelea kuwa mazuri na ya kupendeza.

Kwa sababu ya urafiki ambao mnao, maisha yenu ya mahusiano yatakuwa rahisi na ya kimapenzi. Ya ukaribu  zaidi. sex itakuwa sio kipaumbele chenu bali ni matokeo ya  upendo mlionao. mahitaji yenu ya kimwili yatatosheka kwa pamoja.

7.Utamuheshimu na yeye Atakuheshimu wewe.

Kila mtu anaheshimu mipaka ya mwenzake na mnaweza kuhimizana katika kutimiza malengo yenu. kama unapenda kucheza , atakuhimiza kufanya hivyo. hutahitaji kukamilisha hisia zako zote. atakuwa na mahusiano mazuri na watu wengine pia. Ni mtu muhimu kwako. anakufanya ujisikie vizuri.

8.Malengo yenu yanafanana.

Hutajaribu kumbadilisha. au kujaribu kuomba kuishi na yeye. hutahitaji awe mtu wa kutengeneza kitu chako. ni mtu ambaye ulimtaka awe wako. thamani yake ni muhimu katika maswali hata. Unataka watoto?  Unapenda kusafiri?  Una hamu ya kupata uzoefu fulani?  unakubaliana katika mambo ya pesa?  Una furaha unapokuwa naye?  Unataka kuishi naye  na kuwa naye chumba kimoja?

Afya ya mahusiano yako ni muhimu katika maisha ya ndoa utakayoingia. Lakini hakuna kipimo cha kupimia uzima huo. Ni wewe tu na mwenza wako  mnajua kama mahusiano yatadumu au  yataishia kwenye kona. yatakuwa na matunda  au hapana. Mttajua kama ni  mazuri au sio.  hizo dalili nane zikusaidie kufahamu kama ni ya afya au sio, yatadumu au hayatadumu.

Credit: www.lizzdavid.com

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.