Maswali haya nafahamu yatagusa kila mahali katika mahusiano ambayo yanahitaji ukamilifu,  wakati mtu  anapokaa kwa muda mrefu au kujaribu kutoka na mtu huyu mara mwingine  ni katika kutafuta  mahusiano mazuri, ya kudumu katika maisha yake. Atakupa furaha?  nitakuwa wake peke yangu?  Nitajipenda nilivyo nitakapokuwa naye pamoja?

Hii inaonekana vizuri na nzuri. Kupata mwenze anayekupenda, utakuwa umewekeza kwa undani zaidi, anayekusaidia, anayekuelewa, na anakusaidia kukua  unavyotaka kufikia. kwa hio tatizo liko wapi?

Matarajio yako muhimu yamekuwa sumu katika mahusiano yako?

Wengi huwa na matarajio mengi kutoka kwa wenza wao.  Na wakati huo huo wanahitaji mahusiano ya kudumu yasibadilishe  matarajio yao. ni kama maigizo. wanahitaji mapenzi ya ukamilifu.

Mahusiano yako yanalingana  na  hayo matarajio hapo juu ya kumfanya mtu azimie peke yake? Au wewe ni wale ambao uliingia kwenye ndoa kwa sababu ya huduma ya kukamilisha mahitaji yako ya kiuchumi,  au  ndoa yako imeanza na hisia  za muhimu ya kukamilishana na  kupendana, au  matarajio yako sio kitu cha kukukamilisha lakini  unahitaji kukua  vizuri katika makusudio yako.

Katika maisha ya leo, unatakiwa kujitegemea ,  hapo utatafuta mwenza ambaye atakutana japo na matarajio yako kidogo, ambayo yatawasaidia  katika mahusiano yenu na kuwa na furaha ya kisaikolojia  zaidi kuliko ilivyokuwa pale mwanzo.

Matokeo?  Haya matarajio mapya ya siku hizi  na viwango kwa ajili ya furaha, hayatoshelezi mabadiliko ya ndoa.

Kitu ambacho kiliangaliwa zamani kama ndio furaha ya ndoa,  hayafikii viwango hivyo hata kidogo. Mahusiano haya  hayatoshelezi.

Ndoa Zipo Kwa Ajili Ya Kushindwa? Hapana.  wakati mahusiano ya kawaida yanaweza yasiwe ya kuridhisha ,  mahusiano bora  yanaweza kuwa ya kuridhisha kuliko  yalivyokuwa kabla. Uhusiano wa kawaida una  sifa ya mahusiano ya kisaikolojia ya kipekee yanahitaji nguvu zaidi.  Kama mahusiano yatafikia viwango vya juu,  watu hao wataishi kwa furaha, ni watu positive  na wenye nguvu  ya kupigania mahusiano yao.

Kwa maneno mengine , mahusiano ya watu siku hizi wanajali sana katika kuishi vizuri kuliko kule mwanzo , japo sio wote.  lakini pia wanashikilia mahusiano yenye viwango vya juu, matarajio yao ni kupata mtu  ambaye ana ufahamu kama wao. Wanafanya hivi kutaka kuepuka  pressure mbalimbali,  uzazi usio na ushirikiano, stress mbalimbali n.k.

Kwa Hio Ni Nini Suluhisho? 

1.Pata muda wa kutosha wa kuwepo na mwenza wako.

Hii ni rahisi kwa baadhi ya watu.  Lakini kujifunza hili katika mahusiano, kutanguliza mahitaji ya mwenzako  inaweza kuwa njia ya kusaidia kukamilisha kwa ajili ya kuiridhisha ndoa.

2.Tafuta njia Ya Faida ya Kumpa mwenza wako  ili kuondoa mashaka.

Kama vile kuonyesha shukurani kwa mwenza kwa kila anachokifanya kwako, iwe ni kikubwa au kidogo. itaongeza urafiki wa karibu na wa kimapenzi.

3.Eneza Msaada.

Huenda katika sehemu hii, mahusiano yako yangekuwa yanaridhika zaidi kama ungejifunza kwa rafiki zako  au familia yako   ingekusaidia wewe kukutana na kusaidia wengine, kuwaonea huruma , kuwapenda, kuwajali wengine kama unavyojijali mwenyewe. Kujitolea kwa mambo ya kijamii.

Ukiwa wewe ni mtu wa kutaka viwango zaidi kwenye mahusiano hutaweza kuridhika katika mahusiano yako, utabaki kushuhudia wale wenye kujua kulea  mambo  ya muhimu tu wanayotakiwa kwenye mahusiano. Wewe utabaki na ndoa yenye kuzimia na kuamka , kuzimia mara kwa mara, na baadae kuzimia moja kwa moja. kama hutaki aina hii ya mahusiano jirekebishe , jifahamu vizuri acha kuiga mambo makubwa. kubali mambo ya muhimu  , mengine  yatajileta yenyewe. halafu utaona ndoa yako kuridhika.

Mahusiano yana nafasi kubwa katika maisha yetu, huenda moja ya mabadiliko bora  tunayofanya  kwa ajili ya kuishi kwa kujifunza saikolojia nzuri inayotuwezesha kumuelewa mwingine . kutambua kuwa sisi ni wanadamu na kila mtu ana mapungufu yake.

Credit: www.lizzdavid.com