HomeZezekibubuchallenge

Sababu ya Watu Wengi kushindwa ku save /kuwekeza

Sababu ya Watu Wengi kushindwa ku save /kuwekeza
Like Tweet Pin it Share Share Email

KINACHOSABABISHA wengi wetu kukosa hamasa ya kusave/kuwekeza ni ile hali ya kuiona safari hii kuwa ndefu sana na kufikiria pengine hata tunachokifanya kisije kutunufaisha sisi bali wale waliobaki. Na hii inaletwa na ule mtazamo wa kudhani kusave/kuwekeza ni kwa ajili ya maisha wakati wa “retirement” ambayo definition yake kwetu ni miaka 60. Sasa unaanza kujiuliza, hivi niwekeze kweli miaka yote kwa ajili tu ya kuja kuishi vizuri nikiwa na miaka 60? Yaani miaka yote “nijibane” nisubirie kurelax nikiwa uzeeni? Na kwani nitaishi miaka mingapi duniani? Ukijiuliza maswali ya aina hii ni lazima utakosa motivation, hata ingekuwa mimi. Lakini bahati mbaya hivi sivyo ilivyo.
==
KWANZA- Retirement sio umri bali ni Financial Status. 
Yani pale utakapokuwa na uhuru wa kifedha hata kama ni katika umri wa miaka 35 unaweza ku-staafu.Na maana ya kustaafu sio kuacha kufanya kazi kabisa, bali kuacha kulazimika kufanya kazi kwa ajili ya kipato. Unakuwa na uhuru wa kuamua kufanya kazi au kutofanya kazi. Na utafanya kazi kwa terms zako wewe na kwenye kitu unachokipenda. Sasa hivi tupo wengi tunafanya kazi hatuna furaha nazo ila ni kwa ajili ya kumudu maisha.
Na kuna vitu tunavipenda sana lakini haviwezi kutuingizia kipato cha kutosha mahitaji yetu kwahiyo hatuna choice zaidi ya kuwa tusipopafurahia kwasababu tunahitaji pesa.
==
PILI- Financial Freedom haitafsiriwi kwa idadi ya mamilioni/mabilioni bali pale utakapokuwa na “passive income” kipato cha uhakika kila mwezi kinachotokana na assets/mali ulizoweza kumiliki, ambacho kinazidi mahitaji yako ya mwezi.Mfano mahitaji ni 2 MIL na assets zako zina uwezo wa kukuingizia 2.5 MIL kila mwezi hapa wewe una financial freedom. Assets ni pamoja na (cash, hisa, bonds, mutual funds/UTT, real estate~ nyumba za kupangisha, viwanja etc) mali zinakuingizia pesa hata ukiwa umelala.
==
TATU- Lengo sio kusave/kuwekeza kwa muda usiokwisha. Weka lengo la kuwekeza kama vile unatakiwa ku RETIRE ndani ya miaka kumi. Chagua wewe ni lini kutoka sasa unataka kupata uhuru wa kifedha? Kisha fanya mahesabu kujua kiasi cha kusave/kuwekeza kila mwezi kufikia lengo lako. Click #hesabusip kuona post niliyoelezea jinsi ya kupiga hesabu hizi. UTAFANIKIWA!

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.