HomeNyumbani

NYUMBANI :::TIPS ZA JIKONI ,VIKOROMBWEZO VYA HAPA NA PALE

NYUMBANI :::TIPS ZA JIKONI ,VIKOROMBWEZO VYA HAPA NA PALE
Like Tweet Pin it Share Share Email

Hizi Tips kuna group la whatsApp nipo waliituma na ni vitu vizuri nikasema niweze ku share na nyie wadau maana wamama humu ni wengi,na as they say mwanamke JIKO.

Kitchen hacks zinasaidia kufanya matunzo au mambo ya jikoni yaende vizuri iwe kwenye upishi ,usafi ,shopping etc.

1⃣ Ukimarinate nyama au samaki kwa viungo( vitunguu saum, tangawizi, masala) ongeza mafuta kidogo na mtindi vjk viwili inalainika na kunoga

2⃣ Ukikosa vanila unaweza saga Ganda la limao bichi kuleta harufu nzuri kwenye keki au chapati maji

3.Ukitaka kupika mboga ya karanga, saga karanga kisha tumia maziwa kukorogea karanga badala ya maji inanoga sana

4. Chapat ukiógeza kdg nazi ya unga na ukakandia maziwa chapati inakuwa zaid ya nzuri

5. Ukitaka chips au ndizi ziwe nzuri, chemsha kdg dk 5 ipua zichuje maji then weka kwenye freezer. Ukitaka kukaanga toa pasha mafuta choma usisubiri zitoke barafu, utastaajab radha yake

pic menutime

6. Ukiunguza wali penyeza mapande makubwa ya pilipili hoho ndani ya wali huwa inaondoa kabisa harufu ya kuungua

7. Ukiona mafuta yamekuwa mengi kwenye supu au mchuzi tumia mkate wa siles kupitisha juu kufyonza

8. Ukitaka maharage yawe na rojo zuri,baada ya kubandika tia mafuta ya kupikia yaivie pamoja

9.Ukitengeneza juice ya rosela au ubuyu unaweza weka mchaichai pale unapochemsha juice inavutia sana

10.Chapati ikilala ukitaka kuipasha iwe lain ichove kwenye maji baridi na kuitoa then pasha kwenye frypan bila mafuta..itakuwa kama umepika leo

11.Ukipika matembele ukiweka tangawiz na pilipili manga yanakuwa matamu balaa

12. Juice ya parachichi weka ndimu au limao utaipenda

14. Ukitaka samaki wabichi wasivurugike au kung’ang’ania wkt wa kukaanga. Wapake unga wa ngano wakolee halafu kaanga ni watamu mno

15. Ukitaka kubadili pishi la wali weka kitungú maji, saumu na iliki kdg wkt wa kuchemsha maji then yachuje halafu pika wali wako unanukia balaa

16.Kama unatumia gesi kupikia wali, jaribu tumia maji ya baridi kupikia mchele unanoga hasa

♦17.Ukitaka utumbo uive haraka weka limao pekee bila chumvi kwa yatke maji ya kwanza.

Hizi hacks nimetumiwa tu ,mie nimeongezea na picha ili zinoge ,thanks to my Friend Jaha alotuma kwa group i hope zitawasaidia

Comments (3)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.