HomeShosti talk

Mahusiano : Tatizo Kubwa Ni Kujiona Uko Sahihi Kila Mara.

Mahusiano : Tatizo Kubwa Ni Kujiona Uko Sahihi Kila Mara.
Like Tweet Pin it Share Share Email

Unaweza kubadilisha mawazo yako , Hisia zako, na tabia zako ndani ya mahusiano yako kwa kuelewa  mtindo  uliopo kati yenu na  mtindo wa watu unaohusiana nao.

Kila aina ya mshikamano uliopo  una athari tofauti jinsi ya kushughulikia au kudharau  changamoto za vitisho, sifa zilizopo na  hisia zinazotokea, Na tabia ambazo unajiwekea mwenyewe zinaweza kurekebisha hisia zako.Kwa kuangalia zaidi eneo hili , unaweza kupata kitu unachokitaka  zaidi na kupata kidogo kile ambacho hukitaki ndani ya mahusiano yako.

Ili kumanage hivi vitu ni muhimu  kujifunza kuvunja vitu ambavyo havihitajiki, vitu vinavyokwamisha  furaha , vitu ambavyo kila mara vinatufanya tusielewane, vitu vinavyoumiza.

Ili Ubadili Hisia Zako, Mawazo Yako,mitazamo yako, Na Tabia Zako Ndani Ya Mahusiano, Inaweza Kukuokoa Kutokana Na Kujiona Uko Sahihi Kila Mara. Kubali Wakati Mwingine  Kuwa Sio Sahihi.

Sababu kubwa inayomfanya mtu kujiona  kuwa hana makosa, na kujiona yuko sahihi kwa kila kitu ni kukosa kujitambua. Kukosa kujua jinsi ya kujipenda na kuwapenda wengine. Kutaka kufanyiwa vizuri yeye, bila ya kuangalia wengine. Kiburi ni kitu kinachosababisha mtu kujiona yuko sahihi kila kitu. Ndivyo inavyotokea ndani ya mahusiano.

Kitu Chochote Kinaweza Kuleta Kutoelewana Kama Kila Mmoja Atakuwa Anamchunguza Mwenzake. Kila Mmoja atakuwa anajiona yuko sahihi kuliko mwenzake .

Kwa mfano , mtu anaweza kusema… kila mara yeye anafanya  anachokitaka…Ana njia zake …Hajali ninachofikiria mimi… Mtu mwingine ,anahisi kutoeleweka  na kujiona kama anasingiziwa kitu kuwa amefanya. ”

”Mwingine anasema , sio kweli, mara ya mwisho  nilikuambia tutoke na tukatoka  kwenda mahali ulipotaka tuende.

mahusiano-3 Tatizo Kubwa Ni Kujiona Uko Sahihi Kila Mara

Ndio, hio ni kwa sababu nilikusema sana na kukulazimisha kufanya hivyo.

Kutokana na mabishano hayo,Baada ya muda kidogo utasikia sauti zinabadilika  za kulaumiana na kutupiana maneno mbalimbali . Na hapo utakuta  yanaanza kuletwa hata mambo yaliopita mwaka mmoja huko nyuma , yanachimbuliwa kwa sababu ya hicho kitu kimoja ambacho kimeanzishwa .Sasa kabla hujajua  sehemu zote mbili zinaumia, wanakasirika  na kupata vidonda  moyoni. Na ugomvi huo utaisha tu kama mtu mmoja ataamua kutoka sehemu hiyo.

Vyovyote vile iwe ni wewe ndani ya mahusiano yako , au umesikia  kwa jirani ambao wana mtindo huu . Ni muhimu kuelewa kwamba  kitu walichokuwa wanakisema ni kwa sababu ya hasira.  Kuogopa  kutokana na kukosa usalama, kujiona kuwa mwenzake hamjali hata kidogo.

Ni vizuri kama utaanza kubeba  makosa ya mwenzako, hata kama hukufanya wewe. Ukifanya hivyo utamfundisha na mwenza wako  kubeba ya kwako. Hapo mtaondoa  ubishi wa kujiona kuwa uko sahihi kuliko mwingine.

Upo utani ambao uliweza kutumiwa . I thought i was wrong once, but i was mistaken.

Kunatokea nini mnapokuwa mnalaumiana mara kwa mara?  Utaanza kujiona uko mbali na mwenza wako. utaanza kujiona mpweke japo upo kwenye ndoa.Mwingine atamuona mwenzake mpumbavu, sio mtu mzuri, hafai kwa lolote.

Fikiria kama ndio wewe na mwenza wako  hamuelewani, mmetengana katika mazungumzo yenu. Mwingine anaenda Kulia , mwingine kushoto.

Sote tunajua hawa watu, unaweza kuwa wewe au majirani zako. au inaweza kuwa mimi . Na ukweli ambao tunaweza kufahamu kihakika ni kwamba kila mtu yuko sahihi.Mimi mwenyewe niko sahihi, wewe uko sahihi, mwenza wako yuko sahihi, hata majirani zako wako sahihi.

”Usisikilize ninachosema, sikiliza ninachokimaanisha”

Hata mimi ninaekuandikia hapa ilinichukua muda mrefu kumjua mwenza wangu anachokimaanisha.  Kwa mfano wangu huu.  Kama mtu ataweza kusikia mwenza wake anamaanisha kitu gani. Kwa mfano kama utasikia akisema nasikitika na nina wasiwasi  kwamba huenda hunijali   wala kuniheshimu. Unaweza ukawa uko hivyo lakini kitu cha kusema hapa ni kwamba,  Nakujali sana na nasikitika  kama unaona kitu hicho cha tofauti, niambie nifanyeje ili utambue kuwa nakujali, Ili ujisikie vizuri.

Lakini kama ukikazama na kujiona uko sahihi. Hatakuelewa.

Unaweza pia kujiuliza maswali mengi kichwani mwako , Kwani itatokea nini kama nikimwacha mwenza wangu ajione yuko sahihi?

Kwa maneno mengine , Utapoteza kitu gani  kama  hutabishana naye?  Itatokea nini kama atafikiria ni sawa. mwache ajione yuko sahihi juu yako.

Hakuna cha kushinda hapa, badala yake  ni kutengeneza  umbali kati yenu.

Kwa hio mwache mtu ajisikie hivyo. Achilia na usiwe na hofu kuhusu  usahihi wako ulivyo. kama uko sahihi , ndani yako unajua uko sahihi. Haitakuumiza wewe, Zaidi sana itakupa zaidi unachotaka … Afya na mahusiano  yenye furaha ya kutosha.

Uhuru Wa Mabadiliko.

Umependa makala hii?

CREDIT : www.lizzdavid.com

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.