HomeShosti talk

Mahusiano : Inaumiza Kuwa Mwanamke Mwingine By Lizz David.

Mahusiano : Inaumiza Kuwa Mwanamke Mwingine By Lizz David.
Like Tweet Pin it Share Share Email

Kila mara nilikuwa nikikaa kiti cha nyuma,  Tungeweza kutumia sababu ya kuongea kuhusu hilo, lakini haikuwezekana. Nilifahamu ilikuwaje, Kitu kisichowezekana kisichoweza kuongeleka, kisichofikirika. Mistress. Ndio ilikuwa mimi.

Nilikuwa na hisia nzuri , na nilitaka kuwa naye, na yeye alichukulia advantage. Lakini nitawezaje kumlaumu, wakati nilipokuwa najisikia hatia, lakini bado nilikuwepo naye. Nilipenda uwepo wake, sex, mali,  hata pale nilipoona simu au ujumbe kutoka kwa mwanamke mwingine sikujali. kusikia uko wapi, unarudi saa ngapi iliumiza moyo.

Iliumiza moyo, lakini bado niliganda kwake. kwa kwa sababu nilitaka kutimiza nia yangu.  mawazo yangu , shauku yangu. Nami nilichukulia advantage hio. Kwa hio sikufanya kosa, sikuwa na hatia.  Hata kama nilisikia hivyo moyoni kwa kujua kuwa kuna mwingine.

Kilichokuwa kikiniumiza zaidi ni pale anaposema anaenda  kulala upande mwingine. Moyo ulikuwa unavujia nyonga  yote. maumivu makali. machozi . nikifikiria zamu . Wiki nyingine ni maongezi mapya.

Nilimpenda , kwa sababu ya upole na ukarimu wake kwangu. kwa hio niliweza kuzoea urafiki wa mapenzi kwake, ingawa kuna wakati maumivu . lakini alinipenda sana.Nami niliathiriwa kwake ndio maana niliamua kuweka makao. Akiwepo na mimi hutaweza kuamini kama ana mwanamke mwingine jinsi anavyoonyesha mapenzi.Utafikiri hafanyi kitu upande mwingine.

Kichwani mwangu nilikuwa nikiumia na neno hili Mistress, ingawa hakuna mtu ambaye aliweza kuniita hivyo , zaidi ya kuitwa mke wa pili. Lakini akilini mwangu sikupendelea majina hayo yote, japo nilimpenda yeye.

Kitu kibaya nilichokifanya na hata nikajisikia vibaya ni pale nilipotaka  kuonekana bora kuliko mwenzangu. Lakini asante Mungu moyo wangu ulifahamu hilo na kujaribu kulegeza kamba. Nilipenda kuwa na mavazi mazuri, kuwa na gari nzuri, nyumba nzuri, watoto. na vyote nilipata.

Lakini sikiliza. Mungu aliendelea kusema na mimi .Kuwa nilichokuwa nataka nimekipata, ni wakati wa kuondoka. Sauti hii iliongea kila siku , hata nikasikia kama naumwa. Mbaya zaidi Mwanaume Upendo ndio ulikolea kwangu, lakini hakufahamu kuwa mimi najipanga taratibu kuachilia kamba. Hatimae nilipata Amani ya kuachilia . Baada ya miaka 15 ya pamoja.

Nilianza kuweka akili yangu vizuri, kufundisha ubongo wangu kuwa natakiwa kuondoka. Siku ilipofika nilikaa na huyo mwanamke na kumwambia nia yangu, Hakuamini nilichokuwa namwambia. lakini moyo wangu ulikuwa imara kiasi cha chuma. Niliwaita ndugu na kuwaeleza Nia  yangu. Walibaki kushangaa. walidhani natania . mume wangu hakuamini pamoja na kwamba nilishaanza kumweka vizuri kiakili, kuwa nilitaka  tukae kwa mkataba. hata sijui hili neno nilipata wapi la mkataba. ilikuwa hivyo. Ni hadthi ndefu.

Ninachotaka wewe ufahamu hapa , hasa msichana au dada yeyote ambaye hajaolewa, Usikubali kuwa mistress, Usijiunganishe na hisia hizo zinaumiza kupita maelezo.Utaathirika kisaikolojia, Utaanza kujiuliza maswali ambayo hayana majibu na wala ukitafuta jibu popote hutapata. Kwa nini uwe mke wa pili. Wanaume ni wengi. kata hio hisia kama ipo kwako.  imekuwepo hio toka tukiwa wadogo tunaona, lakini isiwe kwako.  Usifanye hivyo kwa ajili yako.

SOURCE : www.lizzdavid.com

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.