HomeShosti talk

Kwa Nini Unaendelea Kuvutia Mwanaume, Mwanamke Tofauti Na Mahitaji Yako.

Kwa Nini Unaendelea Kuvutia Mwanaume, Mwanamke Tofauti Na Mahitaji Yako.
Like Tweet Pin it Share Share Email

Unaweza ukawa unafanya kila kitu kizuri , unatumia mbinu zote ili kumpata mtu sahihi ambaye umekuwa ukifikiria, ukiota kila siku lakini usimpate 

Sio kosa lako , kipindi bado hakijafika, hujawa tayari, unachotakiwa kufanya ni kujiandaa kikamilifu. watu wengi wanaweza kujitokeza lakini sio wale ambao unawataka.

Swali limekuja, na mimi nimeona vema tufahamu wote ambao tupo kwenye mchakato huu.

Nina miaka 40, nina kazi yangu nzuri, lakini naendelea kukutana na  wanaume ambao sio sahihi, sio ninaowataka. sivai vibaya, navaa nguo nzuri, zinaishia magotini, iwe sketi au gauni, lakini sipati mtu ninaemtaka.sijiachii mwili wangu wazi, na wala sinunui mapenzi, au kudanganya, au kufanya ngono pasi na kusubiri mwanaume wa ndoto yangu, Kitu gani ninachokosea?

Kwa nini kuanza kufikiria kuwa unafanya kitu kibaya? Unaweza au usiweze kuwa unafanya kitu kibaya . Lakini  swali linakuja , Unaangukia kwa mtu ambaye sio sahihi au unavutia mtu ambaye sio sahihi? sio chaguo lako? Sio tegemeo lako? Sio hamu yako? Sio hitaji lako?

Kwa sababu mtu fulani amevutiwa na wewe, huhitaji kuwa naye, huhitaji kukubali. Mtu uliemvutia kwako hana kitu cha muhimu cha kufanya  kwako kulingana na umri wako au hali yako, au jinsi unavyovaa, au kazi nzuri uliyonayo, au upekee wako, umbo lako.

Tatizo ni kwamba sio kuwavutia bali ni wewe unawakaribisha, Hutakiwi kuchagua hao au kukubali kila mtu anayekuja kwako kwa ajili ya mvuto ulionao. Kumvutia mtu inaanzia kwenye tabia  na ujasiri uliopo ndani mwako.

Amua ni mtu wa aina gani unaemtaka na uwe na ujasiri kuwa atakuja  kwako. Kama utaendelea kuwakaribisha wale ambao sio unaowataka , utakuwa unaziba nafasi , na hutampata unayemtaka.

Utakapokutana na huyo mtu hutapata shida ya kumtambua , maana ni mtu ambaye wa aina yako na ambaye ulitaka kuwa naye maishani mwako. Ili kufanikiwa katika hili , sikiliza zaidi kuliko kuongea unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza.Sikiliza na tazama jinsi ambavyo wanawachukulia wengine, kama wanaheshimu watu wa kawaida. wahudumu wanaowahudumia. hio ndio dalili kubwa ya kujua mtu ambaye atakuwa mzuri kwako.

Maana kama anawafanyia watu wengine vizuri hivyo ndivyo atakufanyia wewe.Kumbuka mtu atakapokuonyesha jinsi alivyo. amini ndivyo alivyo.

Anza kujijali, kujikubali, kujipenda mwenyewe, jithamini, uwe una ujasiri, endelea kujiheshimu. Utakapokuwa unafanya haya, yatakurudia wewe .

CREDIT : www.lizzdavid.com

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.