HomeShosti talk

Kama Unataka Mahusiano Yako Yadumu Acha Kufanya Yafuatayo.

Kama Unataka Mahusiano Yako Yadumu Acha Kufanya Yafuatayo.
Like Tweet Pin it Share Share Email

Acha kucheza na moyo wake. Mwanamme kwa mwanamke~

1.Acha kufikiria  kuwa hayatadumu

Ukiwa kwenye mahusiano fikiria kitu kimoja tu–fikiria kila kitu kipo vizuri. acha kusema sijui, sijui.  mara hatuna mabadiliko. acha kusema hamkupata nafasi ya kujuana.

Kama ukiwa positive utamwambukiza na mwenza wako kuwa positive. hamtaweza kuharibu mahusiano yenu. Acha kuwa negative.

2.Acha kucheza game

Una hasira au masononeko au umeumizwa. mwenza wako anauliza. Una tatizo gani?  Kuna kitu kimeniudhi jioni ya leo. Acha ujinga huo, acha utoto, ni mchezo wa game unaoua mahusiano.

Acha kujaribu kutafuta majibu ambayo hayapo duniani. Badala yake  tafuta suluhisho. ondoa maumivu na hasira , kwa sababu hayo mawili  yanadanganya na ni  hisia za hatari  unapojaribu kuzikubali ndani yako.

3.Acha Kufikiria Upendo  Unatosha

n-HAPPY-SENIOR-AFRICANAMERICAN-COUPLE-large570 Kama Unataka Mahusiano Yako Yadumu Acha Kufanya Yafuatayo

Katika safari ya mahusiano  ya watu wawili, Kunatokea mazuri na mabaya , Na wakati mwingine yanatokea mabaya zaidi kuliko upendo. Kuelewana kutawafikisha  mahali pazuri.

Upendo ni kuhusu mvuto. uwajibikaji.Lakini kupenda  ni kuhusu kufurahiana. kuheshimiana  na kuhurumiana.kama utamuona mwenza wako kuwa ni mkarimu na mpole , na wewe unatakiwa kuwa hivyo. uwe naye, ongea naye, kuwa rafiki yake, hapo mtakuwa na kitu cha kushikilia.

4.Acha Wivu.

Kama humwamini kwa nini uliendelea kuwa naye tangu mwanzo?  Na kama anaaminika na wewe una tatizo la yale yaliopita  kwa sababu ya usaliti,  fanyia kazi hilo pamoja kabla mambo hayajaharibika ili kupata heshima na usalama zaidi .Kwa upande mwingine? Kama utajikuta ndani ya mahusiano mahali ambapo mmoja ana wivu na huwezi kurekebisha, imekuwa ndio tatizo kubwa. Ondoka haraka. Kwa sababu wivu sio dalili ya upendo, ni umiliki na kutaka kuonea. Mahusiano ya kudumu yanahitaji Kuaminiana.

5.Acha kutulia kwa kitu ambacho hukitaki

Mahusiano yanahitaji usawa wenye nguvu ya pamoja.  kushirikiana ,sio kumtazama mtu mmoja anateseka  kwa ajili yako halafu huoni kama anateseka.au unafanya kusudi.

Unapomkubali mtu  ambaye hakukutana na mahitaji yako. hutaweza kutulia , hutaweza kuishi kwa furaha kwa muda mrefu. hapo utajikuta unaumwa kwa mawazo na kufa ukiwa bado mdogo. Wenza wenye mafanikio huheshimiana, kila mtu huheshimu thamani ya mwenzake.

6.Acha Kufikiria Unahitaji Mtu fulani ili upate Furaha

Nenda na maisha yako, acha kusubiri, fanya urafiki, Fanya kazi kwa bidii, Safiri, uwe na umbo zuri, kula vizuri, Kuwa na furaha.  Mtu unayemtafuta hataki mtu asiye na furaha, mtu mwenye matatizo, mpweke, na aliyechanganyikiwa.

Kwa kadri unavyoweza kujijali, kujipenda, kujiheshimu, ndio watu watahitaji kuwepo na wewe, kukupenda, kukaa na wewe, Ni muda wa kuacha  baadhi ya tabia mbaya. badilika . anza kuvutia watu kwa  kuwapenda kama unavyojipenda, kuwajali kama unavyojijali. watu watataka kuwa na wewe kwa sababu zote sahihi.

Credit:  www.lizzdavid.com

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.