HomeShosti talk

JISAIDIE MWENYEWE , CHUKUA HATUA UNAPOONA MAPENZI YAMEKWISHA

JISAIDIE MWENYEWE , CHUKUA HATUA UNAPOONA MAPENZI YAMEKWISHA
Like Tweet Pin it Share Share Email

Mbinu za kukusaidia unapotengana na mtu au unapotaka kutengeneza upya mapenzi yenu.

Mnapokutana na mtu na mnapendana, wote mnaona kama mmegusa nyota moja, kwa muda kidogo, mnakuwa mnatembea hewani.

Mara mambo yanabadilika. Inaweza yakawa yanatoka ndani ya mtu au yakawa yanatoka nje ya mtu. Na yanayotoka nje mara nyingi hayawezi kukaa hewani yataanguka. Lakini yanayotoka ndani yanaweza kustamili kukaa hewani.

Namba kubwa ya matatizo haya inatokana na familia, marafiki, wengine Siasa au vyama na hata matarajio.  Lakini bado unaweza kuponya mahusiano yako kama utaachana na hisia mbaya, hasira,  chuki kabla  ya kuchelewa  kufanya hivyo kwa sababu kuvunjika kwa mahusiano ni kazi nguvu .

Weka akilini haya wakati unapoona mahusiano yanaleta shida.

-Kubali kwamba nusu ya ndoa zinaishia kutengana, lakini ya kwako haitaishia hivyo. Itadumu.

-Uwe na ufahamu kwamba watu wanaoishi pamoja bila ya ndoa nao huachana, na hio inaathiri sifa ya maisha.

-Unapohisi tatizo, tafuta muda mzuri wa kurekebisha haraka na mwenza wako.

-Epuka ushauri wa marafiki

-Kama huwezi kutatua tatizo, jaribu kuwa na hadhi

-Inapotokea tatizo na kama itaonekana haliwezi kutatuliwa , achilia ndani yako kipindi cha maombolezo, halafu  Fungua upendo upya

-Kama ukijiona unazidiwa na huzuni, tafuta msaada na upati  tiba.

Kuna ndoa nyingi zinaishi kwa mazoea, utakuta ndani watu wana vyumba tofauti, lakini ni wanandoa. Sijui hio ni ndoa ya aina gani.

Uwe na ufahamu kwamba hata wale wanaoishi bila ya ndoa wanaachana, na bado ni stress.

Kutengana huku kunaongeza huzuni ya kisaikolojia katika maisha ambayo mtu hawezi kutosheka.

Jaribu kuyaponya mahusiano yako kwa utulivu mnapozungumzia hali hio. Kuachana ni Pagumu.

Kama unahisi mahusiano yameingia tatizo na unahitaji kuokoa,  Mawazo haya ni ya kuzingatia.

-Elezea ukweli…kitu fulani hakijakaa vizuri kati yetu

-Elezea hisia zako… unahitaji wote tuwe na jukumu hili au kama sio basi tusonge mbele

-Ukubali kusikiliza…kwa utulivu, kutoka kwa mwenza wako

-Fanyenyi maamuzi wote wawili kwamba mtajaribu tena na tena kujirekebisha. Peaneni muda.

-Kama hamtaweza kupatana, tumieni hadhi zenu

-Kama mmoja ataonyesha kutokubali, badala ya hasira, bado unaweza kuomba muda wa kujaribu tena.

Na wakati ukiwa peke yako, jiulize. kama ulijua mahusiano  mara nyingi mwanamke ndio mwanzilishi, na lakini bado hataki kukubali kurekebisha  . Angalia njia ya pili ya kurekebisha.

Hii itakusaidia kujua kuwa kuna jambo ndani ya mahusiano ambalo linamsumbua mwenza wako. Itakupa urahisi kuachilia kama ukijua.

Fuata process za kupona na kukubali.

Unaweza kujikuta unalia na kuwa na huzuni . tafuta njia ambayo ni nzuri ya kuifuata

-Anza siku na shukurani. Jikumbushe siku nzuri mlizokuwa nazo, na jinsi ambavyo utapata mtu wa kukuthamini tena.

-Kubali majaribu na maongezi mabaya ambayo yatatoka kwa mwenza wako. Ongea mambo mazuri kuhusu yeye.

-Tumia notebook yako kuandika mambo ya shukurani kila siku. Andika vipengele ambavyo ni vizuri kama vile, ujasiri, kusaidia, kupata nguvu, furaha, Nafuu, kutosheka, shukurani na hekima.

-Kama utasikia upweke, tafuta picha zako mwenyewe badala ya kukumbuka picha za ex wako. Focus kwenye kupata mapenzi mazuri

Kuwa makini unapowauliza marafiki ushauri.

Wakati mwingine unatamani kuongea na marafiki zako wote ili kutaka ushauri kwao, lakini kuwa makini kwamba mara nyingi ushauri unaweza kuja kwa maana tatu na kila moja una hatari yake.

-Kama ningekuwa wewe… lakini sio wao

-Kwa upande wangu.

Mara nyingi watu hutoa ushauri kulingana na mazingira yao , kitu ambacho kinaweza kufanana au kisifanane na mazingira yako.

-Watakuambia kitu ambacho unataka kusikia..ni nje ya ushauri mzuri hata kama sio muhimu kwa ajili yako wakati huo watakuambia.

Kitu cha kufanya ni wewe kuangalia chanzo cha tatizo ili uweze kujifunza

Amini mtu wako wa ndani. Ndani yako yupo mshauri aliye bora kuliko yeyote.

Kama umetengana , tenganeni kwa hadhi na msonge mbele

Look ahead to love again.

Panga matarajio

Tafuta upendo wa kweli

Jitahidi usirudie makosa

Kuwa wazi kama bado ni mapema, unaweza kupata mtu wa kumkumbatia na kumpenda pasipo kitendo cha ngono. Ili kusubiri muda maalumu kwa ajili yako.

Credit : www.lizzdavid.com 

Comments (1)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.