HomeZezekibubuchallenge

Jinsi Ya Kuishi Kwa Bajeti and Still Have Some Fun!By Godlisten Katunzi

Jinsi Ya Kuishi Kwa Bajeti and Still Have Some Fun!By Godlisten Katunzi
Like Tweet Pin it Share Share Email

Kwanza kabisa swala la kuishi kwa bajeti huwa ni gumu na wakati mwingine unaweza kuanza na yakakushinda na ukaamua kuacha. Ila kitu kimoja ambacho unaweza kufanya, ni kujifunza jinsi ya kutengeneza bajeti na kuishi kwa bajeti na bado maisha yakawa sawa. Inaweza kuwa ngumu hasa kama ndio umetoka chuo au ndio unaanza kazi, unaweza kuwa unatengeneza laki tano na bado una madeni ya miilioni,  na rafiki yako anatengeneza milioni moja na hana hata deni moja.

Ukweli ni kwamba huwezi kujilinganisha na maisha ya wengine ila kama ukitengeneza bajeti vizuri unaweza kufurahia maisha yako and be happy!

Kuna Vitu ambavyo vinafanya swala la kubajeti kuwa gumu

  • Huna hela
  • Hela uliyonayo haitoshi
  • Kuwa katika hali kutofanya vitu unavyotaka kufanya
  • Kuwa na madeni mengi
  • Kuwa na hofu ya kuwa na madeni

Uzuri wa kuwa na bajeti huwa inakuondolea hofu na kukufanya utenge hela yako kulingana na hela uliyonayo mfukoni ambayo sasa inapelekea kuwa na hali ya amani na kuondoa hofu.

Panga Bajeti Mapema

Kitu ambacho watu wengi tunasahau ni kwamba bajeti ni kama mpango wa utumiaji wa hela zako. Yaani unakuwa unatengeneza jinsi utakavyotumia hela yakokulingana na hela uliyonayo, na kulingana na mahitaji yako.

Mfano utapanga mwezi huu nitatumia laki moja kwenye maswala ya chakula tu.

utatumia elf thelasini kwa ajili ya starehe mwezi huu

Unaponga hivi kwanza unakuwa unajua ni shilingi ngapi utatumia mwezi ujao, unakuwa unajua nini kinaendelea kwenye maswala ya hela zako.

Tumia njia mbadala.

Kwa kawaida sio lazima kila weekend uende out ukaenjoy. kwa hiyo wakati mwingine inabidi uangalie ni njia gani zingine unaweza kutumia kwa ajili ya kuenjoy na bado ukaendelea kuwa ndani ya bajeti yako. Mfano nenda beach tu hapo nauli yako tu ndio itakuwa cost kubwa na kule ukienda ujue kabisa utaenda kunywa vinjwaji vingapi.

Hii ni bora kuliko uende kwenye show ambayo itakubidi ulipie kiingilio, nauli,  na vinywaji juu, hapo lazima utoke nje ya bajeti. Kitu kingine ambacho unaweza kufanya ni kwenda na hela tu uliyopanga kutumia usidishe hela ukasema ni ya emeegency kwa sababu hiyo emmergency inaweza kuwa bia tatu.

Usiogope kusema Hapana

usiogope kusema hapana kwa vitu ambavyo unajua kabisa vitaingilia bajeti yako. Hii ni muhimu sana na hapa ndio watu wengi  tunashindwa kuendelea na mipango yetu kwa sababu unakuwa unajua kabisa mwisho wa mwezi kuna hela itaingia tena benk kwa hiyo unapuuzia mwisho wa siku unajiukuta ulipanga bajeti ila haukuifata kwa sababu tu ulishindwa kujizuia kusema NO. Kwa hiyo kama unaona kabisa hicho kiatu au gauni au hilo bag wala haliendani na bajeti yako wewe tulia.

Hapo Chini Nimekuwekea Titles Ambazo Naona Naweza Kuziandia Articles.

  1. Jinsi Ya Kwenda Out On A Budget.
  • Tabia Na Faida Za Watu Wanatengeneza Bajeti Za Pesa Zao.
  • Jinsi Ya Kujirudi Baada Ya Kuvuruga Bajeti Yako Uliyokuwa Umeipanga.
  • Jinsi Ya Kuanza Kutengeneza Bajeti
  • Hatua Za Mwanzo Unapotaka Kuanza Kusave Hela Zako

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.