HomeNMB Karibu yako

HABARI NJEMA ZA NMB MTOTO AKAUNTI

HABARI NJEMA ZA NMB MTOTO AKAUNTI
Like Tweet Pin it Share Share Email

NMB wana akaunti speacial kwa ajili ya mtoto wako ELIMU YAKE MAISHA YAKE YA BAADAE WAJIBU WANGU.

Hii inakusaidia kupanga na kuongeza akiba yako kwa ajili ya maisha bora ya mtoto wako ya baadae kwa urahisi zaidi.

Vigezo 

Kwa mzazi /mlezi mwenye mtoto wenye umri wa miaka kati ya 0-17.

Kiwango cha chini cha kufungua akaunti ni shillingi 5000 tu au USD,EURO.GBP 5

Haina makato ya uendeshaji wa akaunti ya kila mwezi

Weka kiasi chochote cha fedha kupitia NMB Mobile au NMB waka au Matawi ya NMB na uweze kupata huduma muda wowote.

Pata riba ya ziada ya kuvutia kwa kiwango chochote kilicho kwenye akaunti yako

Pata huduma ya bure ya kuhamisha fedha kwa agizo maalumu (standing order)

Hii akaunti zamani ilikuwa ikiitwa Junior akaunti ambayo sasa ni NMB MTOTO AKAUNTI.

Mahitaji kwa ajili ya kufungua NMB mtoto Akaunti

Ni kwa mtoto mwenye umri chini ya miaka 18

Kitambulisho kinachokubalika cha mzazi au mlezi

Barua ya utambulisho wa mzazi /mlezi kutoka kwa viongozi wa mtaa au kijiji au mwajiri.

Cheti cha kuzaliwa cha mtoto au kiapo cha mahakama au pasipoti ya kusafiria

Picha mbili za mtoto za hivi karibuni zenye kivuli cha rangi ya bluu kwa nyuma

Picha mbili za mzazi/mlezi  za hivi karibuni zenye kivuli cha rangi ya bluu kwa nyuma

Kiwango cha chini cha kunfungua Akaunti cha Tzs 5000 au USD,EURO,GBP 5.

Comments (1)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.