HomeZezekibubuchallenge

Fahamu tofauti kati ya Mkopo Mzuri na Mkopo Mbaya

Fahamu tofauti kati ya Mkopo Mzuri na Mkopo Mbaya
Like Tweet Pin it Share Share Email

FAHAMU tofauti kati ya mkopo mzuri na mkopo mbaya. Mkopo mzuri ni ule unaoweka pesa mfukoni mwako—yani unautumia kufanya kitu ambacho kitalipa mkopo pamoja na riba yake halafu kikupe na faida juu.Mkopo mbaya ni ule unaochomoa pesa kutoka mfukoni mwako. Umechukua mkopo umeweka kwenye kitu ambacho kwanza sio cha msingi (hakikuingizii pesa) na bado unaingia mfukoni kutoa pesa kulipa riba.
==
Hili ni swala lingine ambalo wengi wetu hatuelewi na ni kati ya vitu vinavyoturudisha wengi sana nyuma. Iko hivi—mkopo unatakiwa UKULIPE! Huwezi kujitetea/ kuhalalisha kuchukua mkopo kama haukulipi. Mfano mkopo wa nyumba—utasema unakulipa kama baada ya mahesabu unaona kabisa utaokoa pesa au utatengeneza pesa. Nchi nyingi zilizoendelea mikopo ya nyumba ina riba kidogo sana na hivyo unakuta hata ile pesa unayolipa kodi ni nyingi kuliko ambayo ungelipa kwa mwezi kama ukichukua mkopo. Kwa situation kama hii ni sahihi zaidi kuchukua mkopo kwani unaokoa pesa. Mkopo wa kumalizia nyumba—nao inabidi kufanya mahesabu kwanza kuona kama unaokoa pesa au la, otherwise subiri utamalizia kidogo kidogo. Mikopo mingine mfano kama mkopo wa gari la kutumia huwezi kujitetea kabisa—si sahihi. Mkopo wa kwenda vacation, kununua makochi, kurembesha nyumba —SIO SAHIHI.
Save pesa kwa ajili ya kununua gari,na kufanya hayo mengine sio kuchukua mkopo. Ile riba utakayolipa ni pesa yako inapotea.
==
[MFANO RAHISI] umechukua mkopo wa MILIONI MOJA kwa ajili ya biashara, labda riba yake ni laki moja hivyo jumla ni TZS 1,100,000. Ili tuseme ni mkopo mzuri basi tuweze kuzalisha 1.1Million ya mkopo+riba halafu na faida juu. Kama mkopo unajilipa tu basi hupati kitu nayo angalia kwa makini. Hii ni topic ambayo ni sensitive sana, lakini elewa formula moja tu kwamba mkopo unatakiwa ukulipe. Kama utaweza kujiridhisha kwa aina yoyote kwamba unakulipa basi uko sawa.MAISHA NI MAHESABU!!#smartmoneydecisions#financialeducation#avoiddebt#savetobuy#personalloan#financialindependence#financialpeace#journeytofinancialfreedom2019#financialfreedomchallengetz

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.