HomeCELEBRITY NEWS

Breaking News::: Lulu Atolewa Gerezani ,Sasa Atatumikia kifungo cha Nje

Breaking News::: Lulu Atolewa Gerezani ,Sasa Atatumikia kifungo cha Nje
Like Tweet Pin it Share Share Email

Hii ni good news kwa walio wengi wetu na mashabiki wa Elizabeth Michael aka Lulu,Muigizaji huyu wa Bongo Movie amebadilishiwa adhabu kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania na sasa atatumikia kifungo cha nje.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia .Hukumu ya kesi hiyo ilisomwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, ambaye baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa mawakili wa upande wa mshtakiwa alitoa hukumu.

Lulu, alishtakiwa kwa kesi ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini na nje ya nchi, Steven Kanumba ambaye pia alikuwa mpenzi wake.

source ;Millardayo

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.