HomeMONEY TALK

Aina mbili za Watu duniani watumiaji na wauzaji ,Tabia zao kifedha

Aina mbili za Watu duniani watumiaji na wauzaji ,Tabia zao kifedha
Like Tweet Pin it Share Share Email

Tofauti yetu/watu wa kipato cha kawaida na matajiri ni kwamba sisi wakati wote tunawaza tu kutumia pesa. Wakati wenzetu wanawaza kuzikumbatia pesa zao ili wazitumie katika kuwekeza/kununua assets kwanza zizalishe pesa nyingine.
—————————————
Hii ndio sababu narudia mara nyingi kusema kwamba maisha yana formula na yanahitaji MAHESABU. Ukipata pesa, usipoitumia sasa hivi unaona kama kuna kitu kikubwa unakikosa/unanyimwa uhuru. Lakini hebu tufikirie kidogo, hivi tukipata pesa na kuitumia hapo hapo si inakuwa imekwisha halafu basi tena? Njia sahihi si ingekuwa kuitumia pesa hiyo kama fursa ya kutengeneza pesa nyingine na kuendelea kuvuna pesa kutokana na pesa tuliyoichuma kwa jasho? Tunachagua kila siku kuhangaika kutafuta pesa wakati hatuna uhakika wa kuwa kwenye hali ya kuendelea kuchuma pesa kila wakati? TUTAFAKARI!
—————————————
Hii haimaanishi kwamba tusitumie pesa zetu kwenye mahitaji yetu ya lazima pamoja na mambo kidogo ya kujifurahisha. Bali zile pesa tunazozitumia kununua vitu ambavyo ni unnecessary/liabilities tuziangalie sana maana ni kujichimbia shimo ambalo baadaye itatulazimu kuishi humo.
—————————————
Unapopata pesa yako, hebu waza ni jinsi gani unaweza kuitumia kama fursa ya kuzalisha pesa nyingine na kujiwekea mfumo ambao utakuwa unavuna pesa wakati wote. Hata hivyo kuwa makini sana usije kuwekeza kwenye “fursa” zisizo salama kwa kisingizio kwamba unataka kuzalisha pesa, itakuwa kama kuweka maji kwenye gunia. Epuka kuwa na tamaa, ambayo itakufanya uparamie “fursa” za kitapeli. Usiwekeze kwenye kitu chochote ambacho hakisimamiwi na mamlaka husika kutoka serikali ya Tanzania

Comments (0)

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.